.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 18 Mei 2016

MABINGWA WA LIGI KUU ENGLAND WAENDELEA KULA BATA, WAWASILI THAILAND NA KUPATA MAPOKEZI MAKUBWA

Mlinda mlango wa Leicester City, Kasper Schmeichel, kocha wa timu hiyo Claudio Ranieri na Shinji Okazakiwakiwasalimia waandishi wa habari kwa utamaduni wa wenyeji Thailand " wai " mara baada ya kuwasili nchini humo wakiwa katika ziara mara baada ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu England msimu huu. Tahailand ndipo nyumbani kwa mmiliki wa timu hiyo.
Christian Fuchs kushoto na nahodha wa timu hiyo Wes Morgan wakiwa wenye nyuso za furaha mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Suvarnabhumi, Bangkok mapema leo.
Makamu wa Rais wa Leicester City, Sombat Dechapanichkul akimvisha taji kocha mkuu wa timu hiyo Claudio Ranier
Mamia ya mashabiki wa timu hiyo wakipiga picha pamoja na wachezaji wa Leicester City mara baada ya kuwasili nchini Thailand.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni