.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 18 Mei 2016

MANCHESTER UNITED YASHINDA MCHEZO WAKE WA MWISHO WA LIGI KUU

Dogo Marcus Rashford ametakata wakati Manchester United ikitwaa nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Uropa kufuatia kuifunga Bournemouth mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza usiku wa kuamkia leo.

Mchezo huo wa jana ulishuhudiwa na mashabiki wachache katika dimba la Old Trafford, baada ya jumapili kuhairishwa kutokana na tishio la bomu ambapo baadaye ilibainika kuwa ni bomu feki.

Mkongwe Wayne Rooney alikuwa wa kwanza kuipatia Manchester United goli la kwanza, huku dogo anayekuja juu Marcus Rashford akifunga goli la pili kabla ya Ashley Young kupachika goli la tatu. Bournemouth walipata goli pekee baada ya Chris Smalling kujifunga.
               Ashley Young akiachia shuti lililojaa wavuni na kuandia goli la tatu
   Mashabiki wa Man U wakishinikiza kwa njia ya bango kocha Louis van Gaal aondoke
                 Asanteni kwa Kuja: Kocha Louis van Gaal akiwashukuru mashabiki

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni