Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela alitoa salamu katika Mkutano wa Halmashauri ya BAKWATA wilaya ya Iringa. Katika hotuba yake alzungumzia mambo muhimu 2 , Uongozi na Uchumi katika dini ya Kiislamu. . aliendelea kusema " Kama mjuavyo hatuwezi kuishi bila kuwa na kiongozi mahali popote tutakapokuwa lazima kuwepo na uongozi. Vitabu vyote vya dini vinatoa umuhimu wa kuwepo kwa kiongozi.
Mtume (s.a.w.) ametukumbusha sote kuwa kila mtu ajue kuwa ni kiongozi anayewajibika juu ya wale anaowaongoza na hapana shaka ya kuwepo maulizo ya Allah (s.w.) juu ya uwajibikaji wake juu ya wale anawaongoza.
Aliendelea " kila kiongozi anao wajibu kwa wale anaowaongoza. Katika kipengele hiki tumejaribu kubainisha wajibu wa viongozi wa Kiislamu kama ifuatavyo:
1. Ucha-Mungu
2. Huruma
3. Uadilifu
Mh Kasesela alisistiza kwa kusema kuwa, kiongozi wa Kiislamu anatakiwa awe muaminifu na mkweli na asithubutu kujilimbikizia mali kwa kutumia madaraka yake ya uongozi. Amir au kiongozi wa juu wa Serikali ya Kiislamu anatakiwa achukue mshahara au posho kutoka kwenye mfuko wa serikali (Baitul-mali) kiasi kile tu kinachotosheleza mahitaji muhimu ya chakula, mavazi na makazi kwa yeye mwenyewe na familia yake.
Kiongozi wa Kiislamu anatakiwa akumbuke daima kuwa uongozi katika Uislamu si kitega uchumi kama ulivyo uongozi wa Kitwaghuti. Mtume Muhammad (s.a.w.) ambaye ndiye kiongozi ambaye ni tunajifunza kwa mwenendo na uongozi wake bora, aliishi maisha rahisi.
Kinyume chake viongozi wa Kitwaghuti, huchukua madaraka ya uongozi wanaopewa na jamii zao kama kitega uchumi chao kwa ajili ya kujinufaisha wao binafsi. Huifuja watakavyo na humpa yeyote wamtakaye kwa upendeleo mali ya jamii ambayo imepatikana kwa kukung'uta mifuko ya masikini.
Muda mfupi baada ya kiongozi wa Kitwaghuti kukabidhiwa madaraka ya uongozi wa ngazi ya juu katika jamii, utamuona ana gari zuri jipya ana nyumba nzuri mpya, ana miradi huku na kule na mabadiliko ya kila namna katika matumizi yake ya kimaisha pamoja na familia yake.
Kama mambo yenyewe ni haya, kwa nini watu wengine katika jamii ya Kitwaghuti wasiupupie uongozi kwa hali na mali au kwa kufa na kupona? Kwa nini mtu aliyeonja uongozi katika serikali ya Kitwaghuti asing'ang'anie kubakia humo kwa gharama yoyote ile?
Kama mambo yenyewe ni haya, kwa nini watu wengine katika jamii ya Kitwaghuti wasiupupie uongozi kwa hali na mali au kwa kufa na kupona? Kwa nini mtu aliyeonja uongozi katika serikali ya Kitwaghuti asing'ang'anie kubakia humo kwa gharama yoyote ile?
Kwa nini mapinduzi ya mara kwa mara, rushwa na mauaji yasitegemewe katika jamii za Kitwaghuti ambapo watu wanashindania uongozi kwa lengo la kujinufaisha wao binafsi? Haya yote ni matunda machungu yanayotarajiwa katika jamii kutokana na uongozi uliokosa uadilifu.
Kwa kuwa mwanadamu ni mchanganyiko wa mwili na roho, pia mahitajio yake yamegawanyika, anamahitajio ya kiroho na kimwili. Mahitajio ya kiroho ambayo humuwezesha mwanadamu kuishi maisha ya utulivu yenye furaha na amani, hupatikana kwa kufuata kwa utii na unyenyekevu mwongozo wa Allah (s.w.)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni