Mmoja wa wanafunzi wakike waliotekwa
huko Chibok nchini Nigeria amepatikana, ikiwa ni mwanafunzi wa kwanza
kupatikana tangu miaka miwili kupita.
Mwanafunzi huyo Amina Ali Nkeki
alikutwa jumanne akiwa amebeba mtoto na kundi la wapiganaji
waliojitolea kujilinda akiwa kwenye Msitu wa Sambisa karibu na mpaka
wa Cameroon.
Mwanafunzi huyo alikuwa namtu
anayeshukiwa kuwa ni mmoja wa wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
Wanafunzi wa kike 218 hawajulikani
walipo baada ya kutekwa shuleni na Boko Haram kaskazini mashariki mwa
Nigeria Aprili 2014.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni