.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 19 Mei 2016

SEVILLA YAIFUNGA LIVERPOOL NA KUTWAA KOMBE LA LIGI YA UROPA

Timu ya Liverpool imejikuta ikipoteza mchezo katika kipindi cha pili na kuiwezesha Sevilla kutwaa Kombe la Ligi ya Uropo kwa mara ya tatu mfululizo katika mchezo uliochezwa jana usiku.

Kikosi cha kocha Jurgen Klopp kilionekana kama kimejipanga kutwaa kombe hilo katika mchezo huo wa fainali wakati Daniel Sturridge alipofanya shambulizi nzuri na kuipatia Liverpool goli la kuongoza.

Kazi hiyo nzuri ya ya Sturridge ilikuja kutibuka katika sekunde 17 za mwanzoni mwa kipindi cha pili baada ya Kevin Gameiro kuutumbukiza wavuni mpira wa krosi iliyopigwa na Mariano Ferreira na kuisawazishia Sevilla. Sevilla iliongeza magoli mengine mawili kupitia Andújar Moreno Coke.
                  Daniel Sturridge akipiga mpira kwa guu la kushoto na kujaa wavuni
               Muuaji wa Liverpool Andújar Moreno Coke akipachika goli lake la pili 
                Daniel Sturridge akiwa amekaa chini uwanjani asiamini kilichotokea

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni