.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 1 Mei 2016

SWANSEA YAICHAKAZA LIVERPOOL NA KUJIOKOA KUSHUKA DARAJA

Timu ya Swansea City imekichakaza kikosi cha Liverpool kilichokuwa na mabadiliko makubwa kwa ushindi wa magoli 3-0 na kujiokoa kushuka daraja katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Goli la kichwa lililofungwa na Andre Ayew na kisha baadaye goli safi la Jack Cork yaliwafanya wenyeji Swansea kuongoza katika kipindi cha kwanza kwa magoli 2-0.

Christian Benteke alifunga goli lililowapa matumaini Liverpool, lakini goli la pili la Ayew katika mchezo huo lilimaliza matumaini ya Liverpool.
                                     Andre Ayew akishangilia goli lake la kwanza alilofunga
Christian Benteke akinyoosha vidole juu kumshukuru Mungu baada ya kufunga goli

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni