.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 6 Mei 2016

TIMU YA LIVERPOOL KUVAANA NA SEVILLA FAINALI YA LIGI YA UROPA

Kocha Jurgen Klopp anaonekana kuelekea kutwaa kikombe chake cha kwanza katika msimu huu akiwa na Liverpool baada ya kuishinda Villarreal na kutinga fainali ya Ligi ya Uropa.

Ikiwa imefungwa goli moja katika mchezo wa awali, Liverpool ilisawazisha kupitia goli la mapema la kujifunga la Bruno Soriano.

Daniel Sturridge, aliyeachwa katika mchezo wa Hispania, aliipatia Liverpool goli la pili Liverpool kwa mpira wa chini, ikiwa ni kazi nzuri iliyofanywa na Roberto Firmino na Adam Lallana akaongeza la tatu.
                                       Daniel Sturridge akipachika goli la pili la Liverpool 
                                   Adam Lallan akifunga goli la tatu katika mchezo huo 
Timu ya Sevilla inaendelea vyema katika jitihada zake za kutwaa kwa mara ya tatu mfululizo ubingwa wa Ligi ya Uropa baada ya kuifunga Shakhtar Donetsk na sasa itakutana na Liverpool kwenye fainali.

Baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Ukraine, Sevilla ilianza vyema mchezo huo wa pili kwa kufunga goli kupitia kwa Kevin Gameiro, kabla ya mchezaji wa zamani wa Arsenal Eduardo kusawazisha.

Gameiro tena aliipatia Sevilla goli la pili baadae Mariano Ferreira kuongeza la tatu na kufanya matokeo kuwa Sevilla 3-1 Shakhtar Donetsk.
                         Mariano Ferreira akifurahi goli la tatu la Sevilla alilofunga

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni