.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 27 Mei 2016

WAZIRI MAHIGA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akimkaribisha Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga kwenye mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere.
Mhe. Waziri Mahiga akiwahutubia watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara.Katika hotuba yake aliwaasa watumishi kuwa waadilifu, kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuhakikisha shughuli za kidiplomasia zinafanyika kwa tija ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Sera ya Mambo ya Nje inatekelezwa na kuifanya Tanzania kuendelea kupaa katika medani za kimataifa
Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akitoa taarifa ya utangulizi wa mkutano kwa Mhe. Waziri, TUGHE-Taifa pamoja na wafanyakazi waliohudhuria Mkutano huo hawapo pichani. Pia alitumia fursa hiyo kumkaribisha Mhe. Waziri ili aweze kufanya ufunguzi wa Mkutano ambapo tukio hilo liliambatana na utoaji wa zawadi za wafanyakazi bora wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Sehemu ya Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba
Sehemu ya Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Abdallah Kilima akitoa neno la shukrani kwa Waziri Mahiga kwa niaba ya wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Pamoja na kuahidi kufanyia kazi nasaha zilizotolewa, Balozi Kilima alimpongeza Waziri Mahiga kwa kuwa kiongozi bora na wa mfano wa kuigwa na Watumishi wote katika utendaji wa kazi.
Mjumbe kutoka TUGHE-Taifa Bw. Arcado Nchinga pia alizungumza na Watumishi wa Wizara ambapo aliwahimiza kuendelea kufanya kazi kwa juhudi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanaiwakilisha nchi vizuri katika mataifa mengine.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki, Bw. Nigel Msangi akitoa taarifa ya wafanyakazi bora wa Wizara wa mwaka 2015/2016 kwa Waziri Mahiga ambao walitunukiwa zawadi katika mkutano huo
Afisa Habari katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Ally Kondo ndiye aliyeibuka Mfanyakazi Bora na Hodari wa iliyokuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Pichani akipongezwa na Mhe. Waziri Mahiga
Afisa TEHAMA katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw.Salum M. Nalolah ndiye aliyeibuka Mfanyakazi Bora na Hodari iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Pichani akipongezwa na Mhe. Waziri Mahiga
Picha ya pamoja Mhe. Waziri Mahiga na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni