.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 30 Juni 2016

BIBI AHUKUMIWA ADHABU YA KIFO KWA KUMUUA MJUKUU ALIYEMUIBIA SUKARI GURU

Bibi mmoja nchini Kenya amehukumiwa adhabu ya kifo kwa kosa la kumuua mjukuu wake aliyemuibia sukari guru, kwa kushirikiana na baba wa mjukuu huyo.

Bibi huyo Margaret Licha na mtoto wake wa kiume Polycarp Yogo wametiwa hatiani na mahakama kwa kumuua Derickson Onyango. Hata hivyo Yogo ambaye ni baba wa Onyango alifariki dunia kabla ya kutolewa hukumu hiyo.

Wawili hao wanadaiwa kumfunga kamba marehemu Onyango kwenye mti na kumpiga, kumwagia mafuta ya taa na kisha kumuwasha moto kama adhabu ya kuiba sukari guru ya shilingi 5 za Kenya huko Ndhiwa, Homa Bay mwaka 2014.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni