Kocha Mkuu wa
timu ya taifa ya Mpira wa Miguu ya Wanawake Tanzania, Nasra Juma ametangaza
majina ya wachezaji 23 watakaounda kikosi cha Twiga Stars.
Kikosi hicho
kinatarajiwa kwenda Kigali, Rwanda Julai 15, 2016 kucheza mchezo wa kirafiki wa
kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Rwanda ikiwa ni mwaliko maalumu wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Rwanda (Ferwafa).
Wakati Ferwafa
likiingiza mchezo huo wa Julai 17, 2016 kwenye orodha ya michezo inayotambuliwa
na Shirikisho la Mpira na Miguu la Kimataifa (Fifa), lakini Mheshimiwa Rais wa
Rwanda Paul Kagame kuwa sehemu ya burudani ya burudani mbele ya wageni wake
ambao ni wakuu mbalimbali wanaounda Umoja wa Nchi za Afrika (AU) ambao watakuwa
na mkutano wao nchini Rwanda.
Mbali ya soka
kama burudani, pia Rais Kagame atatumia mchezo huo kama hamasa kwa wakuu wa nchi
ili kutoa kipaumbele kwenye soka la wanawake ambako kwa sasa ni ajira ambayo
inakwenda sambamba na kuitikia wito wa kupambana na changamoto za malengo ya millennia
(MCC) ambayo pia yanataka wanawake wapate nafasi.
Makipa:
- Fatma Omary
- Belina Julius
- Najiat Abbas
Walinzi:
Viungo:
- Donisia Daniel
- Amina Ali
- Amina Ramadhani
- Fatuma Bashiri
- Wema Richard
- Fadhila Hamadi
- Mwajuma Abdallah
- Anna Hebron
- Sophia Mwasikili
Washambuaji:
- Tumaini Michael
- Johari Shaaban
- Fatma Idd
- Shelder Bonifdace Mafuru
- Asha Saada Rashid
- Mwanakhamisi Omar
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni