Kikosi cha wachezaji 23 wa timu ya
taifa ya Uingereza kimepokelewa na makaribisho ya zulia jekundu
wakiwasili kwa ajili ya michuano ya Euro 2016 kaskazini mwa mji wa
Chantilly nje ya Jiji la Paris nchini Ufaransa.
Kocha Roy Hodgson amewasili na timu
yake kwenye uwanja wa ndege wa Paris Airport-Le Bourget mapema leo
mchana baada ya kutoka Luton leo asubuhi tayari kwa kushiriki
michuano hiyo ya Mabingwa wa Ulaya siku ya Ijumaa.
Wayne Rooney akishuka kwenye ndege baada ya kutua nchini Ufaransa
Kocha Roy Hodgson akiwa ndani ya Ufaransa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni