Watu
watatu wanaosadikiwa kuwa ni magaidi wakiwa na silaha wametekeleza
mashambulio katika mlango wa kuingilia katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Atatuk mjini Istanbul nchini Uturuki, ambapo katika
shambulio hilo watu 36 waliuawa na wengine wengi wakijeruhiwa.
Magaidi
hao waliokuwa na silaha aina ya AK-47 walifyetua risasi hovyo kwa abiria uwanjani hapo kabla ya wao wenyewe kujiua kwa kujilipua kwa mabomu.
Shirika la ndege la Turkish Airline ni mdhamini mshirika katika fainali za Euro 2016 zinazoendelea huko nchini Ufaransa.
Moja ya bunduki aina ya AK-47 iliyokuwa ikitumiwa na mmoja wa washambuliaji hao
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni