Lionel Messi ameombwa kufikiria upya
uamuzi wake wa kujiuzulu kucheza kimataifa na mchezaji nyota mkongwe
wa zamani wa Argentina Diego Maradona pamoja na rais wa nchi yake.
Mshambuliaji huyo, 29, alitangaza
kujiuzulu kuichezea Argentina baada ya kukosa penati katika fainali
za Copa America na kupoteza nafasi ya kushinda michuano mikubwa kwa
mara nne ndani ya miaka tisa.
Maradona amesema kuwa wale wanaosema
Messi aache kuichezea Argentina wanataka kuona namna taifa hilo
litakavyotumbukia katika hali mbaya ya matokeo ya kisoka.
Huko Jijini Buenos Aires limetambulishwa
sanamu la Lionel Messi, huku rais wa Argentina akisema atakutana na
Messi wiki ijayo kumshawishi abadili msimamo wake.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni