Mfanyakazi wa kampuni ya ndege ya
Virgin amejikuta akipigwa na butwaa baada ya kukutwa akiwa ameuchapa
usingizi na Mmiliki wa Kampuni hiyo Richard Branson.
Mfanyakazi huyo aliyekuwa katika timu
ya wafanyakazi wa dharura, alikutwa akiwa amejikunja kwenye kochi
akiuchapa usingizi kwenye ofisi ya Virgin, Australia Jijini Sydney.
Mmiliki wa Virgin kabla ya kumuamsha
aliamua kupiga naye picha na kisha kumstua mfanyakazi huyo ambaye
hakuamini macho yake na kuzania kuwa anaota.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni