.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 26 Juni 2016

POLAND YATINGA ROBO FAINALI YA EURO 2016 KWA MARA YA KWANZA

Nchi ya Poland imetinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Euro 1016 kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo, baada ya Grzegorz Krychowiak kufunga penati muhimu, katika ushindi uliopatikana kwa mikwaju ya penati 5-4 dhidi ya Switzerland.

Katika mchezo huyo mchezaji mpya wa Arsenal Granit Xhaka alijikuta akivunjika moyo baada ya kuwa mchezaji pekee aliyekosa penati katika mchezo huo huko Saint-Etienne, kwa kupiga mpira nje ya goli.

Mchezo huo uliingia katika hatua ya mikwaju ya penati baada ya mchezaji wa timu ya Stoke City Xherdan Shaqiri kufunga goli bora kwa sasa katika michuano hiyo kwa kuupiga mpira kwa tiki taka na kufanya matokeo yawe 1-1.
                                          Granit Xhaka akipiga nje ya goli mkwaju wa penati
             Xherdan Shaqiri akipiga mpira kwa staili ya tiki taka na kusawazisha goli

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni