Mshambuliaji
Romelu Lukaku amefumania nyavu mara mbili wakati Ubelgiji ikipata
ushindi wake wa kwanza katika michuano ya Euro 2016 na kuichakaza
Jamhuri ya Ireland kwa magoli 3-0.
Baada
ya kipindi cha kwanza kuisha bila ya kupatikana goli, Romelu Lukaku,
alifunga goli lake la kwanza katika michuano hiyo kwa kutumbukiza
mpira pembeni mwa goli la Jamhuri ya Ireland.
Mchezaji
Axel Witsel alifunga goli la pili la Ubelgiji kwa kichwa katika
dakika ya 61, kabla ya Romelu Lukaku tena kuachia shuti lililojaa
wavuni kufuatia kufanywa shambulizi la kushtukiza.
Romelu Lukaku akiachia shuti lililozaa goli la tatu kwa Ubelgiji
Axel Witsel akishangilia goli lake alilofungwa kwa kichwa
Romelu Lukaku akitokwa na machozi baada ya kufunga goli la kwanza akiwa anashagilia na mdogo wake Jordan




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni