
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo mwakilishi wa kampuni ya Shamo World Foundation amesema kuwa wameguswa kutoa msaada katika kituo hicho kwa kutenda matendo ya huruma wakati wa kipindi hiki cha Mwezi wa Ramadhani kwa watoto kwa kuwa wanamahitiji mengi pia ni kuwapunguzia ugumu wa maisha walezi wa watoto hao.
Nae Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre, Zainabu Maunga amewashukuru kampuni ya Shamo World kuwaona kwa jicho la pekee na kwenda kuwapa msaada katika kituo hicho.
Mwakilishi wa Kampuni ya Shamo World Foundation, Salama amesema kampuni hiyo wamekabidhi Kg 50 za Mchele, Kg 50 za unga wa ngano na unga wa ugali, Kg 50 za sukari pamoja na Maboksi 15 ya Tende pamoja na mafuta ya kupikia


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni