Mkurugenzi wa Taasisi ya Nitetee, Flora Lauwo akipungia mkono alipokuwa akitambulishwa bungeni Dodoma.
Flora Lauwo akitafakari jambo alipokuwa akifuatilia mwenendo wa mijadala ya Bunge mjini Dodoma.
Serikali imetakiwa kuziangalia kwa jicho la tatu ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kuanza kutoa ruzuku kwa taasisi za watu binafsi zinazofanya kazi ya kufuatilia na kubaini matatizo yanayowakumba wananchi kama afanyavyo, Flora Lauwo Mkurugenzi wa Taasisi ya Nitetee.
Licha ya serikali kutambua mchango unaotolewa na taasisi hizo, jamii nayo imeaswa kujitokeza kuwasaidia watu ambao wamekuwa wakisumbuliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia ,maradhi na wale wanaohitaji msaada wa kupata elimu .
Kufatia serikali kutambua mchango huo baadhi ya wadau kutoka sekta binafsi wanajitokeza na kubainisha changamoto zinazowakumba. Yapo malengo yanayowekwa na wadau hao ili kutimiza ndoto za kuwasaidia watanzania
“Lakini wapo Wajanja ambao wamekuwa wakinufaisha na misaada wanayopewa na wafadhili badala ya kuwasaidia walengwa,” alisema Lauwo.
Taasisi ya nitetee inajishughulisha na utatuzi wa matatizo yanayozikumba familia zinazoishi katika mazingira magumu ambapo mpaka sasa imeshazifikia kaya 36 pamoja na kuwapeleka watoto 20 shule.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni