Ujerumani imeboresha nafasi yao ya
kuweza kutwaa kombe la michuano ya Euro 2016 kwa kuichakaza Slovakia
kwa magoli 3-0 huko Lille na kutinga robo fainali ya michuano hiyo.
Beki wa kati Jerome Boateng
aliwapatia mabingwa hao wa dunia goli la kuongoza kwa shuti murwa la
umbali wa yadi 25 kabla ya Mario Gomez kufunga goli la pili.
Julian Draxler, ambaye alitoa pande
zuri la goli la pili alifanya matokeo kuwa 3-0 kwa shuti la karibu na
mwamba baada ya mapumziko. Mesut Ozil alikosa penati katika dakika ya
14.
Jerome Boateng akiachia shuti lililojaa wavuni na kuandika goli la kwanza
Golikipa Kozacik akipangua penati iliyopigwa na Mesut Ozil
Eden Hazard amefunga goli zuri la
jitihada binafsi wakati Ubelgiji ikiisambaratisha Hungary kwa magoli
manne kwa bila, na kutinga hatua ya 8 bora ya michuano ya Euro 2016
ambapo sasa watakutana na Wales.
Katika mchezo huo mchezaji wa
Tottenham Toby Alderweireld aliifungia Ubelgiji goli la kwanza na
kisha Michu Batshuayi kuongeza la pili, Hazard alipachika la tatu na
Yannick Carrasco akikamilisha karamu.
Michu Batshuayi akiruka sarakasi kushangilia goli alilofunga
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni