Vifo katika tukio la mashambulizi ya
uwanja wa ndege wa Ataturk Jijini Istanbul vimeongezeka na kufikia
watu 41 ambapo 13 miongoni mwao ni wageni.
Gavana na Jiji hilo la Uturuki
amesema pia majeruhi wameongezeka na kufikia watu 239. Tukio hilo
limetokea jana baada ya washambuliaji watatu kuanza kuwafyatulia watu
risasi.
Magari ya kubebea wagonjwa mahututi yakijipanga kuchukua majeruhi na watu waliouliwa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni