Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) wakifanya usafi katika mazingira ya Hospital ya Temeke mwishoni wa wiki iliyopita katika maadhimisho ya shamrashamra za kilele cha wiki ya usalama na afya kazini zilizoanzia kiwandani kwa matembezi ya hisani kuelekea katika hospitali ya Temeke ambapo wafanyakazi hao walifanya usafi katika mazingira ya hospitali hiyo wakishirikiana na Kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Temeke na timu yake
Usafi ukiendelea katika mazingira ya Hospitali ya Temeke ambapo pia wafanyakazi wa SBL mapema wiki iliyopita ikiwa ni moja ya shughuli za kijamii pia walijitolea kuchangia damu na kupima afya zao katika Hospitali hiyo
Wafanyakazi wa kiwanda cha Bia Serengeti wakiwa katika picha ya pamoja mapema wiki iliyopita mara baada ya kufanya usafi katika mazingira ya Hospitali ya Temeke
Meneja wa Usalama na Afya kazin wa SBL Bwana David Mwakalobo akimkabidhi vifaa vya usafi Kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Temeke
Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda cha bia Serengeti (SBL) akichangia damu ambapo zoezi hilo la kuchangia damu liliambatana na shamrashamra za kilele cha wiki ya usalama na afya kazini zilizoanzia kiwandani kwa matembezi ya hisani kuelekea katika hospitali ya Temeke
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni