Timu za taifa za Wales na Uingereza
zimetinga hatua ya mtoano ya michuano ya Euro 2016 baada ya
kukamilisha michezo yao ya mwisho ya kundi B, katika michuano hiyo
inayofanyika nchini Ufaransa.
Katika mchezo wao wa jana usiku
Wales wasioogopa kitu waliifunga Urusi magoli 3-0 na kuongoza kundi
hilo, huku Uingereza ikishika nafasi ya pili baada ya kutoa sare tasa
na Slovakia.
Wales waliandika goli la kwanza
kupitia kwa Aaron Ramsey, na kisha Neil Taylor kupachika la pili
kabla ya Gareth Bale kufunga la tatu, na kumfanya aongoze kwa kufunga
magoli mengi katika michuano hiyo.
Mshambuliaji nyota Gareth Bale akiifungia Wales goli la tatu
Jamie Vardy akipiga ngumi mwamba wa goli kwa hasira baada ya kukosa goli
Wayne Rooney akionyesha kuchanganyikiwa baada ya goli kukoswa




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni