Wenyeji
Ufaransa wametoka nyuma na kufanikiwa kuifunga Jamhuri ya Ireland,
ambayo ilimaliza mchezo wa robo fainali ya Euro 2016 ikiwa na
wachezaji 10, na kulala 2-1.
Jamhuri
ya Ireland ilianza kwa kushtukiza na kuongoza katika dakika ya pili,
baada ya Robbie Brady kutumbukiza golini mpira wa penati baada ya
Shane Longo kuchezewa rafu.
Hata
hivyo Ufaransa walisawazisha kupitia kwa Antoine Griezmann, kabla ya
baadaye kufunga goli la pili la ushindi.
Olivier Giroud akimshika mkono Antoine Griezmann baada ya kufunga goli la kusawazisha
Antoine Griezmann mwenye jezi namba saba akipachika goli la pili la Ufaransa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni