.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 28 Julai 2016

CHADEMA KUFANYA OPERESHENI UKUTA NCHI NZIMA, MBOWE ASEMA WAPO TAYARI KWA KAZI.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari.
Viongozi mbalimbali wa Chadema wakionyesha ishara ya UKUTA.

Baada ya kufanya kikao cha siku mbili hatimaye Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa tarifa ya kikao hicho pamoja na kutangaza makubaliano ambayo wameyafanya kupitia kikao hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kupitia kikao hicho wamekubaliana kuanzisha operesheni ambayo itafanyika kwa nchi nzima na kuwaagiza viongozi wa wilaya zote nchini wa Chadema kuanza vikao kujiandaa na operesheni hiyo.

Alisema kuwa operesheni hiyo ina lengo kupingana na ukandamizaji wa haki na demokrasia nchini ikiwepo kuzuiwa kufanya mikutano na hivyo kupitia operesheni hiyo ambayo itaandamana na mikutano wataweza kufikisha ujumbe wao kwa serikali kuhusu masikitiko yao ukandamizwaji wa haki na demokrasia.

“Tumefanya makubaliano ya pamoja kuwa Septemba, 1 tutafanya mikutano nchi nzima na mimi kama mwenyekiti nawaagiza viongozi wa chama wa kila wilaya kuanza kujiandaa na mikutano hiyo,

“Operesheni hii imepewa jina la UKUTA ikiwa na maana ya Umoja wa Kupinga Udikteta nchini sio iwe mtu mmoja ndiyo anakuwa na sauti kila jambo anataka kuliongoza yeye hizi ni dalili za udikteta,” alisema Mbowe.

Aidha alisema kuwa katika kutimiza azma yao wamejipanga kuhakikisha operesheni hiyo inafanyika na wapo tayari hata kama vyombo vya usalama vitataka kuingilia kati na kuwazuia.

“Ukiuliza kama nimejipanga na vyombo vya usalama unadhani nimejipanga na nini? tupo tayari na kila jambo na tumeamua ukiuliza tutafanyaje, ukitaka kuvuka mto subiri ukifika mtoni, tupo serious,

“Eti kwa sababu Mwingulu Nchemba amesema kuzuia mikutano wote tutulie … hili tamko tungelitoa tangu Novemba mwaka jana tukategemea tungeona busara lakini tunaona ubabe tu,” alisema Mbowe. Kwa hisani ya Mo Blog

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni