.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 9 Julai 2016

DC GONDWE ATAKA WAFANYABIASHARA KUWEKEZA KWENYE KILIMO KIKUBWA WILAYANI HUMO


MKUU wa wilaya ya Handeni MkoaniTanga,Godwin Gondwe amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanawekeza kwenye kilimo kikubwa cha kisasa ambacho kitakuwa na tija kwao ili kuweza kusukuma gurudumu la maendeleo na kukuza uchumi.

Gondwe alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wafanyabiashara, viongozi wa dini ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka kuona umuhimu wa kutumia fursa ya uwepo wa rutuba nzuri ya ardhi iliyopo wilayani humo kujikita kulima kisasa ili kuweza kupata mafanikio.

Alisema kuwa lazima wafanyabiashara watambue kuwa kilimo ndio njia pekee
ambayo inaweza kuwainua kiuchumi na kuharakisha kasi ya ukuaji wa
maendeleo iwapo watazingati na kukipa kipaumbele kila wakati “Niwaombeni suala la kilimo mlipe msukumo mkubwa sana kwani hii ndio njia pekee ambayo inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kusukuma gurudumu la maendeleo kwa wilaya yetu “Alisema.

Aidha pia alisisitiza umuhimu wa wananchi wa wilaya hiyo kutilia mkazo
kulima mazao yanayostahimili ukame ikiwemo Alizeti, Ufuta,Viazi na
Mihogo ili kuweza kukabiliana na tatizo la kutoku patikana mvua za uhakika kwa ajili ya kilimo cha mahindi.

“ Ninajua katika kipindi hiki tumelima kwa wingi lakini hali ya hewa
sio nzuri na mvua nazo zimekuwa hazipatikana kwa uhakika hivyo lazima
wakulima tubadilike kwa kuanza kupanda mazao yanayostahimili ukame ili
kuweza kuepukana na baa la njaa “Alisema DC Gondwe.

Sambamba na hayo,Mkuu huyo wa wilaya alizishauri taasisi za kibenki
wilayani humo kuhakikisha zinatoa kipaumbele kwa wawekezaji wa kilimo
ili waweze kuzalisha kwa wingi mazao ambayo yataweze kuinua kiuchumi
lakini pia kuchangia pato la Taifa.

Hata hivyo ,Mkuu huyo wa wilaya alitumia pia fursa hiyo kuwaasa wakulima waliopata mazao kidogo kuhakikisha wanayatunza na kuacha kuyauza kwani kufanya hivyo kutaweza kusababisha hali ya njaa kwao.

Naye Shehe wa wilaya ya Handeni, Shabani Mohamed alisema kuwa wao
watamuombea dua Mkuu huyo wa wilaya ili mungu amuwezeshe kuweza kutimiza majukumu yake ipasavyo na kusaidia kuchangia juhudi za maendeleo kwa wananchi.

“Nikuambie Mh Mkuu wa wilaya ujio wako hapa Handeni watu wengi
wamefurahi sana kwani uchapakazi wako unafahamika tokea ulipokuwa
unafanya kazi kwenye kituo cha ITV na tunaamini uhodari huo pia
utasaidia kuinua uchumi wetu “Alisema.

Alisema kuwa wao watahakisha wanampa ushirikiano wa hali ya juu ili
kumuwezesha kutekeleza vema majukumu yake ya kuipa maendeleo wilaya
hiyo. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni