.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 8 Julai 2016

HUAWEI YALETA SIMU ZA KISASA ZENYE UWEZO WA 4G KWA GHARAMA NAFUU

Balozi wa Huawei Jennipher Lazaro, akimuonyesha mteja Catherine Mosha ubora wa simu ya Huawei Y 3lite alipotembelea banda la tigo katika maonyesho ya Sabasaba.
 
Dar es Salaam, Julai 2016;. Kampuni ya Huawei wakishirikiana na makampuni ya mtandao wa simu Vodacom, Airtel na Tigo wamezindua promosheni kwa ajili ya wananchi wote watakaohudhuria maonyesho ya Saba Saba katika matoleo yake ya simu za kisasa za Y3II, Y3 C, na toleo mahususi la Y3 Lite. Katika maonyesho hayo, wananchi wataweza kujipatia simu mpya halisi kwa bei rahisi zaidi

Tukizingatia kwamba kila Mtanzania anayo haki ya kuendelea kuunganishwa na ndugu, jamaa na marafiki kwa njia ya mawasiliano ya simu bila kujali tofauti zao za kipato, Huawei kwa mara nyingine inafanikisha hilo kwa kuleta simu zake za Yseries ili kuwezesha upatikanaji wa simu za kisasa za gharama nafuu kwa watumiaji wa simu wa kipato cha chini Tanzania.

Huawei Tanzania kwa kupitia mkakati wake huu wa kushirikiana na makampuni ya mawasiliano; Tigo, Vodacom na Airtel inampa mtumiaji fursa ya kugusa, kuhisi na kufurahia namna za kipekee za utendaji wa matoleo haya ya Y series ikiwamo Y3II, Y3Lite, Y3 C na Y6 Pro.

Akizungumzia kuhusu ofa na punguzo hili la simu, Meneja Masoko wa Huawei Tanzania Bi. Jane Wang amewahimiza wananchi wote watakaofika katika maonyesho ya Saba Saba kutembelea mabanda ya Vodacom, Tigo na Airtel katika viwanja vya Mwalimu Nyerere kuanzia tar 28 June mpaka tar 8 Julai ili kujipatia moja ya hayo matolea ya simu za Huawei.


”Ofa ya Huawei na Vodacom ni katika simu ya Huawei Kishkwambi kwa gharama y ash. 100,000 ambapo mteja atajipatia kifurushi cha bure cha dakika 1000 na interent GB6 kwa muda wa miezi 12.” Alisema.

Promosheni ya Huawei na Tigo huwawezesha wateja kununua simu ya Huawei Y3 Lite kw ash. 125,000 tu, ikiwa na kifurushi cha GB 2 za data pamoja na muda wa maongezi wa thamani ya sh. 10,000 kwa muda wa miezi 6. 


Kwa Y3II Tigo inatoa ofa ya GB 10 na dakika 3000 kwa kupiga Tigo – Tigo na dakika 500 kupiga mitandao mingine kwa muda wa miezi 3. Y3 C inakuja na dakika 100 za kupiga mitandao yote, kifurushi cha internet cha GB1 na sms 10,000 kwa miezi 4 kutoka Airtel”

Akizungumzia kuhusu simu za gharama ya chini na uhitaji wake kwa watu wa kipato cha chini, Mkurugenzi wa Mauzo wa Huawei Tanzania, Bw. Sylvester Manyara alisema, ukiziangalia simu hizi ni vigumu kuamini kuwa ni simu za gharama ya chini kwa sababu simu zote zimeundwa kwa muundo na teknolojia ya hali ya juu na ya kimataifa. 


Y3 Lite inafaa Zaidi kwa ajili ya watu wazima, wanafunzi na watu wa kipato cha kati na cha chini ambao kwao gharama na utendaji wa simu huwa na umuhimu sawia. 

Simu hii inawafaa wale ambao wanahitaji kuitumia simu kwa muda mrefu sana bila kuichaji. Ni moja ya simu pekee katika zenye thamani hii zinazoweza kuvumilia matumizi makubwa. Betri yenye uwezo mkubwa ya Huawei Y3 Lite inayohifadhi nguvu kwa kiwango cha juu inaiwezesha simu hii kudumu na chaji kwa zaidi ya siku nzima.


Simu ya Huawei Y3 Lite ina kamera yenye uwezo maradufu wa megapikseli 2 katika kamera yake ya mbele na megapikseli 5 ukilinganisha na hizi zingine, ambazo kamera yake ya mbele kwa kawaida ni megapikseli 0.8 na ya nyuma ni megapikseli 2 na taa mbili za kamera ambazo huwezesha mwonekano mzuri wa picha hasa zinazopigwa katika mazingira yenye giza. Simu ya Huawei Y3 Lite ina uwezo mkubwa wa kupiga na kuboresha picha na sauti.

Huawei Y3II si tu ni simu yenye teknologia ya juu, lakini pia inamwoneka wa kipekee pia. Simu hii huja na aina tofauti za mtindo wa rangi. Huawei Y3II inayo kasi kubwa ya kushusha mafaili au picha kwa kasi inayofikia hao MB 21 kwa dakika inayowaezesha watumiaji kuperuzi kurasa za Facebook, Instagram na Whatsapp kwa haraka. Kwa mujibu wa Bw. Manyara, simu ya Y3 II imekusudiwa kwa ajili ya watanzania wa kipato cha chini kabisa na cha kati ambao huhitaji kufurahia maisha, lakini pia hujali kuhusu gharama huku wakihitaji bidhaa bora, ya gharama nafuu na inayodumu.

“Kwa mujibu wa tafiti zetu, vijana wa kisasa hupenda hupenda kusikiliza muziki kwa sauti na kujivinjari na marafiki.Y3II inaokoa muda kwa kuweza kupangilia njia za mkato za kwa matumizi kwa kufuata hatua tatu tu rahisi kama vile, kubofya, kubofya mara mbili, au kubofya kwa muda”. Alisema Bw. Manyara.

Akiyazungumzia matoleo ya Huawei Y Meneja wa Huawei nchini Tanzania Bw. Huxiangyang Jacko amethibitisha kuwa Huawei wanazo bidhaa sahihi kwa kila aina ya mteja, ikijumuisha teknologia ya kiwango cha juu, ubunifu, utendaji mzuri na mwonekano bora kwa bei poa.

“Tumepanga kutengeneza simu zenye kiwango cha juu zaidi zinazokuwezesha kufanya mambo mengi zaidi siku nzima. Tumefanya hivyo katika Y6 Pro ambayo ilizinduliwa mwezi Mei na pia katika matoleo mbalimbali ya simu za Y series yaliyozinduliwa mwezi huu. Matoleo ya Y ni mahususi kwa ajili ya watumiaji wa simu za kisasa”.

Akielezea juhudi zinazofanywa na Huawei, Bw. Edmund Gulay mfanyabiashara aliyetembelea maonyesho ya Saba Saba alikuwa na furaha kuona Huawei wamekuja na matoleo ya Y kwa gharama nafuu na simu imara za kisasa za Y3II, Y3Lite, Y3 C and Y6Pro hususani katika kipindi hiki ambacho kila mtanzania anaharakisha kupata simu orijino katika nchi yetu ambapo wengi wao ni watu wa kipato cha chini na cha kati.

Katika nyakati hizi ambazo watanzania wanauhitaji wa simu bora na zinazodumu, huku TCRA wakiendela na zoezi la kuzima simu zisizo halisi, na katika hitaji la kuweza kufikiwa bila ngarama kubwa kulingana na mahitaji ya kila siku ya kimaisha na shughuri za kibiashara, matoleo ya Y ya Huawei ndio chaguo pekee la watanzania.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni