Wachezaji wa timu ya soka ya Iceland
wamepokelewa kishujaa baada ya kurejea kutoka katika michuano ya Euro
2016, huku maelfu ya mashabiki wao wakiwa mitaani ya mji Reykjavik
kuwashuhudia.
Timu hiyo ilienda Ufaransa ikiwa ni
moja ya taifa dogo kabisa kuwahi kushiriki michuano ya Euro, likiwa
na wananchi wapatao 332,529.
Hata hivyo Iceland haikujali ugeni
wala udogo katika michuano hiyo kwani ilifanya vyema hadi kutinga
robo fainali ambapo ilitolewa na Ufaransa kwa magoli 5-2.
Wachezaji wa Iceland wakiwa juu ya basi lao wakishangiliwa na mashabiki wao
Wachezaji wa Iceland wakiwapungia mikono mashabiki wao kuwashukuru kwa mapokezi makubwa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni