Jose Mourinho amefanya mkutano na
waandishi wa habari tangu chukuliwe kuwa kocha Manchester United na
kuahidi kuwa anahitaji kombe la Ligi Kuu ya Uingereza.
Kocha huyo ametambulishwa rasmi leo
asubuhi kuwa mrithi wa kocha Louis van Gaal, hakumung'unya maneno kwa
kusema Manchester United ilipoteza dira ya ushindi.
Kama hiyo haitoshi Mourinho hakusita
kumtupia kijembe kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kwa kuwa na ukame wa
makombe kwa muda mrefu.
Waandishi wa vyombo vya habari wakimsikiliza kocha Jose Mourinho
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni