.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 3 Julai 2016

JUMUIYA YA SHIA WAMKABIDHI MADAWATI RAIS WA ZANZIBAR, DK. SHEIN

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir Mhe,Mohamed Raza Daramsi wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akifuatana na Viongozi na Mashekhe wa jumuiya hiyo kwa ajili ya kukabidhi msaada wa madawati 100 kwa ushirikiano na familia ya Rais wa Jumuiya,msaada huo utaowanufaisha wanafunzi wa Skuli mbali mbali za Zanzibar
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma akitoa shukurani kwa Uongozi wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir wakati ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kukabidhi madawati 100 kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) ikiwa ni katika kuimarisha sekta ya Elimu hapa Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mashekhe wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir (kulia) Sheikh Shaaban Hussein,Sheikh Maulana Dhishan Haidar na Rais wa Jumuiya hiyo Mhe, Mohamed Raza (kushoto) wakati walipofika ikulu Mjini Zanzibar kukabidhi msaada wa madawati 100 kawanafunzi wa Zanzibar
Rais wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir Mhe,Raza (kushoto) akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia aliyekaa) wakati Jumuiya hiyo ilipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kukabidhi madawati 100 kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar ikiwa ni katika katua za kuimarisha sekta ya Elimu nchini
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia)akikabidhiwa madawati 100 kutoka kwa Viongozi wa jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir na familia ya Rais wa Jumuiya hiyo Mohamed Raza walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,msaada huo kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar, 02/07/2016.[Picha na Ikulu.]

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni