Timu
ya Vijana ya Kenya, imefuta ziara yake ya kwenda Dar es Salaam kwa
ajili kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya vijana wa
Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kwa jina la
Serengeti Boys.
Mchezo
huo ulipangwa kufanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Julai 23,
2016.
Kwa
mujibu wa barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Kenya (FKF), Robert Muthomi kwenda Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), kufuta kwa ziara hiyo kunatokana na nafasi ambayo
Kenya imeipata.
Timu
ya Taifa ya Vijana ya Kenya imeteuliwa kushiriki michuano ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu la COSAFA inayotarajiwa kuanza Julai 22,
2016 hadi Julai 31, 2016 mara baada ya Msumbiji kujitoa kwenye
mashindano hayo.
“Tunaomba
kukutarifu kuwa timu yetu imetuliwa katika michuano ya vijana ya
COSAFA, hivyo ziara yetu Tanzania haitakuwako kama ambavyo sisi
wenyewe tuliomba mchezo huo kwenu (TFF) ufanyike Julai 23, 2016,”
ilisema sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Muthomi.
Licha
ya kwamba mchezo huo hautakuwako, ratiba ya Serengeti Boys ambayo
inapambana kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa Afrika hapo
mwakani, imebaki vilevile kwa timu kuingia kambini Jumapili Julai 17,
2016 kwenye Hosteli za TFF zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume,
Ilala jijini Dar es Salaam.
Timu
hiyo inayonolewa na Bakari Shime itapiga kambi ya wiki moja katika
hosteli hizo, kabla ya kwenda Madagascar ambako itapiga kambi ya
takribani wiki mbili ikiwa ni ahadi ya Rais wa TFF, Jamal Malinzi
ambaye alitoa ofa hiyo baada ya kuwatoa Shelisheli kwa jumla ya mabao
9-0 katika mechi zake mbili za kimataifa.
Serengeti
Boys inatarajiwa kucheza na Afrika Kusini kati ya Agosti 5, 6 au 7,
2016 huko Afrika Kusini kabla ya mchezo wa marudiano utakaofanyika
saa 9.00 alasiri, Agosti 14, 2016 kwenye Uwanja wa Azam Complex,
ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Mshindi
wa jumla katika michezo hiyo, itacheza na timu mshindi kati ya
Namibia na Congo-Brazaville.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni