Kocha
mpya wa Chelsea, Antonio Conte, amesema mshambuliaji Diego Costa
atabakia katika klabu hiyo kwenye msimu ujao, na ni muhimu katika
mipango yake.
Mchezaji
huyo wa kimataifa wa Hispania amekuwa akihusishwa na kurejea katika
klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid.
Costa
mwenye umri wa miaka 27, amefunga magoli 36 katika michezo 77
aliyoichezea Chelsea tangu ajiunge nayo mwaka 2014.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni