Kocha
Pep Guardiola amepata ushindi wake wa kwanza akiwa na Manchester City
baada ya kufikia hatua ya penati dhidi ya Borussia Dortmund katika
mchezo uliochezwa nchini China.
Kipa
wa Manchester City Angus Gunn, 20, aliokoa penati ya Mikel Morino na
kuihakikishia ushindi wa penati 6-5 baada ya mchezo kuishia kwa sare
ya 1-1 huko Shenzhen katika dimba la Longgang.
Katika
mchezo huo mchezaji wa Dortmund Christian Pulisic, 17, alisawazisha
katika dakika za mwisho, na kufanya matokeo kuwa moja kwa moja baada
ya awali Sergio Aguero kuifungia goli la kwanza la mchezo huo.
Kipa wa Manchester City Angus Gunn akipangua penati iliyoipa ushindi timu yake
Wachezaji wa Manchester City wakifurahia ushindi baada ya kipa Gunn kupangua penati
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni