Mwanamuziki
nyota wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Koffi Olomide amefunguliwa
shtaka la kushambulia na kumuumiza dansa wake wa kike katika mahakama
Jijini Kinshasa.
Mashtaka
hayo yamefunguliwa siku tatu kupita tangu atimuliwe Kenya baada ya
video ya tukio hilo kusambazwa kwenye mitandao ya jamii akionekana
akimpiga teke mwanamke.
Maafisa
polisi walimkamata Koffi nyumbani kwake Kinshasa ambapo walimfunga
pingu na kisha kuondoka naye kwenye gari lao, ambapo baadaye
alifikishwa mahakamani.
Iwapo
atatiwa hatiani Koffi Olomide anaweza kufungwa jela miaka mitano.
Mwaka 2012 alipewa adhabu wa kifungo cha uangalizi cha miezi mitatu
baada ya kumpiga prodyuza wake.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni