Mamlaka
za nchini Kenya zimemuondoa kwa nguvu nchini humo mwanamuziki nyota
barani Afrika Koffi Olomide baada ya tukio la kumpiga teke dansa wake
mwanamke.
Tukio
hilo lililonaswa kwenye picha za video Jijini Nairobi katika uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, liliibua hasira za wananchi
kwenye mitandao ya jamii.
Olomide,
anayetokea nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, alikanusha
kumshambulia dansa wake saa chache baada ya tukio hilo, hata hivyo
alikuja kukamatwa baadae na polisi.
Koffi
Olomide aliyekuwa afanye tamasha lake jana Jijini Nairobi,
alisafirishwa na kurejeshwa Jijini Kinshasa nchini DRC, akiwa na
wachezaji wake shoo watatu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni