Maandamano yanaendelea katika miji
kadhaa ya Marekani dhidi ya vitendo vya polisi weupe kuwauwa watu
weusi kwa risasi, kufuatia vifo vya watau wawili hivi karibuni huko
Minnesota na Louisiana.
Barabara zilifungwa na makombora
kurushwa huko Minnesota, wakati wafusi wa kundi lenye silaha la
wanachama wa New Black Panther walipokuwa wakipambana na polisi eneo
la Baton Rouge, Louisiana.
Makumi ya watu wamekamatwa lakini
hata hivyo kwa jumla maandamano yamefanyika kwa amani. Hali pia ni ya
hofu huko Dallas, ambako polisi watano wameuwawa na mtu mwusi
aliyekuwa na silaha wakati wa maandamano.
Mmoja wa waandamanaji akiwa ameshikiliwa na polisi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni