Mamlaka za Jiji la Lagos nchini
Nigeria imeyafunga makanisa 70 na misikiti 20 kwa katika mikakati
yake ya kupunguza kiwango kikubwa cha kelele jijini humo.
Kampeni hiyo ya kukabiliana na
kelele pia imezikumba hoteli 10 pamoja na klabu za starehe, katika
Jiji la Lagos lenye watu milioni 20.
Serikali imeahidi kuhakikisha
inataka kulifanya Jiji hilo la Lagos kuwa halina kelele ifikapo mwaka
2020, kwa kudhibiti kelele za mziki, honi za magari na kutoka kwenye
makanisa na misikiti.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni