Mchungaji
nchini Zimbabwe aliyekamatwa kwa muda baada ya kuratibu mgomo wa
kitaifa wiki iliyopita ametoa wito kwa watu kuendelea kugoma.
Mchungaji
Evan Mawarire ameiambia BBC kuwa watu wanapaswa kuendelea kukaa
nyumbani, kama njia ya kampeni dhidi ya rushwa, uchumi mbovu na
ukosefu wa ajira.
Mchungaji
Mawarire ambaye aliachiwa jana na mahakama baada ya kutupilia mbali
mashtaka yake, amesema kampeni hiyo imejidhatiti kuleta mabadiliko
nchini humo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni