Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mh. Seleman Jaffo amefanya ziara katika halmashauri ya Iringa ambapo alipokelewa na Mkuu wa wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela akiongozana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa Mh Stephen Mhapa.
Katika ziara hiyo alikagua miradi ya maendeleo na kufungua miradi ya vyoo katika shule ya msingi Mikongati tarafa ya Kalenga, maabara ya zahanati ya Kising'a na madarasa ya shule ya sekondari Mikongati.
Pia alizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Iringa. Katika hotuba yake Mh Jafo alisistiza suala la upendo kazini na kujenga nidhamu katika utendaji. Pia aliwaomba wananchi watunze miradi iliyo kamilika ili idumu muda.
Akimkaribisha Naibu Waziri, Mheshimiwa Kasesela aliomba seriakli kuharakisha fedha ili kukamilisha miradi ya maji na barabara, pia kuomba uwezekano kila barabara zinapo jengwa yatengwe maeneo kwa ajili ya emergence unit ili kuokoa miasha ya watu mara ajali zinapotokea.
Aiendelea " leo Mh waziri umezindua maabara hapa Kising'a lakini eneo hili lipo barabara kuu ya kuelekea Dodoma ajali zinapotokea tunapata tabu sana kuokoa maisha ya wananchi ni muhimu sasa Tanroads wana disign barabara mpya ziwepo pia fedha za kujenga vituo vya dharura ambavyo vyawezwa kuunganishwa na vituo vya kupumzikia wananchi ili halmashauri zetu zipumue mara yatokeapo majanga".
Pia akiongea kwenye mkutano wa watumishi Mkurugenzi wa halmashauri Bwana Robert Munyusi pamoja na Katibu tawala wilaya ya Iringa Bwana Robert Chitinka wote kwa pamoja walimpongeza Naibu waziri kwa kasi kubwa ya utendaji kazi wake.
Ziara ilimalizika kwa kumtembelea Mwalimu aliye fiwa na mwanae wakati ziara ikiendelea. Naibu waziri aliwafariji wafiwa na kutoa ubani kisha kuendelea na safari kuelekea Dodoma.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni