Moto
mkubwa wa nyika unaosambaa kwa kasi umewalazimisha mamia ya watu
kukimbia makazi yao katika eneo la mlimani la kaskazini mwa Los
Angeles, California nchini Marekani.
Moto
huo umesambaa katika eneo la hekari 20,000 hadi jana usiku, na
kusambaza moshi mkubwa katika kaunti ya Los Angeles.
Watu
wapatao 300 wameondolewa katika makazi yao karibu na mji wa Santa
Clarita, huku mabwawa ya kuogelea ya umma yaliyopo Pasadeana na
Glendale yakifungwa kutokana na kuzingirwa na moshi na kujaa majivu.
Watu wakikimbia kunusuru maisha yao kufuatia kububuka kwa moto huo wa nyika
Vikosi vya zimamoto vikihaha kukabiliana na moto huo
Ndege ikiwa angani ikimwaga kemikali za kuzima moto
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni