Msanii Jacquiline Wolper (katikati) ambaye mwaka jana alikuwa mmoja wa wasanii wapiga debe wa aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa, akikaribishwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) na Mwenyekiti Mstaafu wa chama hicho, Jakaya Kikwete baada ya kutangaza kujiunga na CCM akitokea Chadema juzi usiku wakati wasanii wakitumbuiza wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Dodoma. (PICHA NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA)
Wolper akifurahi kujiunga CCM ambapo alisema anaomba asamehewe kwa kitendo chake cha kumpigia kampeni Lowassa mwaka jana
Msanii Jacquiline Wolper akifurahi alipokuwa akikaribishwa na Mwenyekiti mstaafu, Jakaya Kikwete baada ya kutangaza kujiunga tena na CCM akitokea Chadema jana usiku wakati wasanii wakitumbuiza wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni