Mwanariadha mlemavu wa Afrika
Kusini, Oscar Pistorius, amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela, kwa
mauaji ya mpenzi wake mwaka 2013.
Hukumu hiyo imekuja baada ya
kutenguliwa kwa hukumu ya awali ya mauaji kutokusudia kufuatia rufaa
iliyokatwa na mwendesha mashtaka Desemba mwaka jana.
Pistorius mwenye miaka 29,
alimfyatulia risasi mara nne na kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp
aliyekuwa amejifungia chooni nyumbani kwake Februari 24, mwaka 2013.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni