Paul
Pogba anatarajia kuwa mchezaji wa Manchester United kwa mara nyingine
tena baada ya kukubalika mpango wa kumnunua kwa paundi milioni 100
kutoka Juventus jana usiku.
Hii
inamaana kuwa mchezaji huyo aliyeondoka Old Trafford kwa kiasi sawa
na bure atarejea kwenye klabu hiyo kwa kusaini mkataba unaoweka
rekodi nchini Uingereza.
Mpango
huo wa kumnasa kiungo huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23,
unatarajiwa kukamilishwa hii leo baada maafisa na wanasheria wa
Juventus kukutana jana huko Turin.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni