Raia
wa Kenya waliofanikiwa kuondoka Sudan Kusini, wameelezea hali ya
mateso waliyopitia baada ya kuibuka mapigano ya wanajeshi watiifu kwa
rais na wale watiifu kwa makamu wa rais Jijini Juba.
Wamesema
kuwa walilazimika kulala chini ya vitanda pamoja na watoto wao,
wakati mapigano yalipoibuka na wakati wote huo mambo yalikuwa magumu
mno kwao na wamepoteza kila kitu.
Mmoja
wa raia hao wa Kenya Millicent Anyango ambaye ameletwa kwa ndege hadi
nchini Kenya amesema hawakuwa na chakula Sudan Kusini, pia
waliporwa kila kitu pamoja na fedha zao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni