Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi imeeleza kuwa
- BODI YA MAPATO (ZRB)
Kwa
mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 14 cha sheria ya Bodi ya
Mapato ya 1996, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bwana Amour Hamil Bakar kuwa
Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar. Bwana Amour Hamil Bakar anachukua
nafasi ya Bwana Abdi Khamis Faki ambae anastaafu kwa mujibu wa Sheria.
Utezi huo unaanza tarehe 1 Agost 2016.
Aidha
kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 15(1) (A) cha sheria hiyo
kama ilivyorekebishwa na kifungu 11 cha Sheria Namba 2 ya mwaka 2000,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali
Mohamed Shein amemteua Bibi Khadija Shamte Mzee kuwa Naibu Kamishna wa
Bodi ya Mapato ya Zanzibar. Bibi Khadija Shamte Mzee anachukua nafasi ya
Bwana Hafidh Ussi Haji ambae uteuzi wake umefutwa.
Uteuzi huo unaanza tarehe 25 Julai 2016.
2.TUME YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA
Kwa
mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 8 cha Sheria ya Tume ya
Maadili ya Umma Namba 4 ya 2015, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bwana Said
Bakari Jecha na Bibi Sebtuu Mohammed Nassor kuwa Makamishna wa Tume ya
Maadili ya Viongozi wa Umma.
Uteuzi huo unaanza tarehe 25 Julai, 2016.
- BODI YA SHIRIKA LA MAGAZETI YA SERIKALI
Kwa
mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 11(1)(a) cha Sheria ya
Shirika la Magazeti ya Serikali Namba 11 ya 2008, Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein
amemteua Bibi Umi Aley kuwa Mwenyeki wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika
la Magazeti ya Serikali.
Uteuzi huo unaanza tarehe 25 Julai 2016.
- TUME YA UTANGAZAJI
Kwa
mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Tume ya
Utangazaji ya Zanzibar Namba 6 ya 1997, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Dkt. Ali
saleh Mwinyikai kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utangazaji ya Zanzibar.
Uteuzi huo unaanza tarehe 25 julai 2016.
- BARAZA LA SANAA NA SENSA YA FILAMU NA UTAMADUNI
Kwa
mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 5(1)(a) cha Sheria ya
Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu na utamaduni Namba 7 ya 2015, Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed
Shein amemteua Bibi Maryam Mohamed Hamdan kuwa mwenyekiti wa Baraza la
Sanaa na Sensa ya Filamu na Utamaduni.
Uteuzi huo unaanza tarehe 25 Julai 2016.
- BARAZA LA MITIHANI LA ZANZIBAR
Kwa
mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 4(1) cha Sheria ya Baraza
la Mitihani la Zanzibar Namba 6 ya 2012, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bibi
Maryam Abdalla Yussuf kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Zanzibar.
Uteuzi huo unaanza tarehe 25 julai 2016.
- SHIRIKA LA VIWANGO LA ZANZIBAR (ZBS)
Kwa
mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 8(2)(a) cha Sheria ya
Shirika la Viwango la Zanzibar Namba 1 ya 2011, Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein
amemteua tena Profesa Ali Seif Mshimba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Shirika la Viwango la Zanzibar.
Uteuzi huo unaanza tarehe 25 julai 2016.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABRI MAELEZO ZANZIBAR.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni