Rais
Francois Hollande wa Ufaransa ataongoza mkutano wa kujadili
mashambulizi ya kigaidi na waziri wa mambo ya ndani kufuatia
shambulizi la Alhamisi Mjini Nice lililouwa watu 84.
Bw.
Hollande, ambaye amesema shambulizi hilo ni la kigaidi, tayari
ameongeza muda wa hali ya tahadhari katika taifa hilo kwa miezi
mitatu.
Alhamisi
dereva mwenye lori aliligonga kwa makusudi kundi la watu wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Bastille katika eneo la ufukweni la Promenade
des Anglais.
Polisi
walifanikiwa kumuua kwa risasi dereva huyo ambaye ametambulika kuwa
ni Mohamed Lahouaiej-Bouhlel, 31, raia wa Tunisia.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni