Rais
wa Ufaransa Fancois Hollande anakutana na viongozi wa Kikristo,
Kiyahudi pamoja na Buddha, baada ya kutokea mauaji ya Padri kanisani
hapo jana huko Normandy.
Padri
huyo Jacques Hamel aliuwawa wakati akiendesha ibada ya asubuhi
kanisani kwa kuchinjwa kwa kisu na watu waliovamia kanisa hilo.
Mmoja
wa washambuliaji hao amebainika kuwa ni Adel Kermiche, 19, ambaye
aliwahi kufungwa jela na aliachiwa nje akiwa chini ya uangalizi wa
polisi.
Shambulizi
hilo limekuja siku 12 tu kupita baada ya shambulizi la Nice ambalo
watu 84 waliuwawa.
Baaada
ya kukutana na viongozi wa dini, rais Francois Hollande atafanya
mkutano wa ulinzi na baraza la ulinzi, na kisha baadaye kukaa na
baraza la mawaziri.
Padri Jacques Hamel wakati wa uhai wake kabla ya kuuwawa kikatili
Adel Kermiche mmoja wa vijana anayehusishwa na mauaji ya Padri Jacques Hamel
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni