Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina (katikati) akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Helene Weesie wakiongozana kuelekea kwenye bomba la kudhibiti wa majitaka ambalo linalenga kuhakikisha kiwango cha juu kiafya kwa kampuni, mazingira na wakazi wa maeneo yaliyo karibu. Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya bia ya Serengeti, John Wanyancha akifafanua jambo kwa wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa bomba la majitaka ambalo lilizinduliwa na Mhe. Luhaga Mpina Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira mapema leo katika kiwandani hapo mapema leo. Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina , Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Helene Weesie na waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini jinsi mtambo wa kusafirisha majitaka unavyofanya kazi kutoka kwa mmoja wa wasimamizi wa mradi huo. Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina (katikati) akifurahi jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Helene Weesie mara baada ya kukata utepe katika mtambo kusafirisha majitaka katika hafla iliyofanyika mapema leo kiwandani hapo.
Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina akiwasha mtambo wa kusafirisha majitaka kiwandani hapo mara baada ya kuzindua rasmi katika hafla iliyofanyika katika kiwanda hicho Temeke Jijini Dar es salaam. Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa bomba la kudhibiti majitaka katika kiwanda cha bia cha serengeti wakifuatilia kwa makini Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina akiongea na wafanyakazi wa kiwanda cha bia ya serengeti mara baada ya uzinduzi wa bomba la kudhibiti majitaka katika kiwanda hicho Jijini Dar es salaam.
Dar es Salaam, Julai 19, 2016- Kampuni ya Bia ya Serengeti leo imezindua bomba la kudhibiti wa majitaka ambalo linalenga kuhakikisha kiwango cha juu kiafya kwa kampuni, mazingira na wakazi wa maeneo yaliyo karibu.
Bomba hilo limejengwa chini ya usimamizi wa Kampuni ya Maji Safi na Taka ya Dar es Salaam (Dawasco), Mamlaka ya Barabara (Tanroads) na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke likihusisha takribani kilometa mbili kuanzia katika kiwanda cha bia cha Serengeti kilichpo Temeke hadi Kurasini ambako ndip ulipo mfumo wa majitaka wa Dawasco.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, huo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Helene Weesie, alisema kwamba mradi huo wa aina yake na wa kwanza nchini unadhihirisha juhudi zisizo na ukomo za kampuni hiyo katika kuhifadhi mazingira.
“Ubora wa maji ni jambo lililo mstari wa mbele katika utengenezaji wa bia lakini suala la usafi kutokana na kuzalishwa kwa majitaka ni sehemu kubwa inayotujengea hisia za kimazingira katika shughuli za kutengeneza bia. Kwa hiyo uzinduzi wa bomba hili ni moja ya hatua ya kusonga mbele katika kuhakikisha yanakuwepo mazingira safi kiafya,” alisema Weesie.
Mkurugenzi Mtendaji huyo alibainisha kwamba majitaka yanayotolewa na bomba hilo yatakuwa yanafanyiwa tiba kwanza ili kuondoa aina yoyote ya sumu kabla ya kuachiwa ili kuingia katika mfumo wa majitaka wa Dawasco.
Alisema kuwa uzinduzi huyo uko katika mkondo mmoja na sera ya Kampuni ya Serengeti ya kujikita katika ustawi wa jamii ambayo imeainishwa katika maeneo manne ya vipaumbele ambavyo vinajumuisha, Utoaji wa Stadi za Maisha, Uendelevu wa Mazingira na Kuboresha Unywaji wa Kistaarabu.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Masuala ya Muungano na Mazingira, Mh. Luhanga Mpina aliipongeza Serengeti kwa kuzindua bomba hilo akibainisha kwamba ujenzi unaendana na ajenda ya serikali ya uhifadhi wa mazingira.
Mpina alibainisha kwamba uchafuzi wa mazingira katika miji na maeneo ya pembezoni unaathiri afya za watu wengi na kupunguza tija inayotokana na mazingira na kutoa wito kwa makampuni mengine kuiga kazi nzuri ya Kampuni ya Bia ya Serengeti katika kuhifadhi mazingira.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni