Timu ya Mpira wa Miguu Ufukweni ya Tanzania imepangwa kucheza na Ivory Coast kati ya Agosti 26, 27 au 28, 2016 kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2017 zitakazofanyika Lagos, Nigeria. Mchezo wa marudiano unatarajiwa kufanyika kati ya Septemba 16, 17, au 18.
Fainali za Mpira wa Miguu Ufukweni ambazo zitafahamika pia kama 2016 CAF Beach Soccer Championship, zitafanyika kuanzia Desemba 13 hadi 18, 2016 jijini Lagos, Nigeria kwa kushirikisha timu nane.
Tayari Nigeria imepasishwa kuwa mshiriki kwa sifa ya uenyeji waketi timu nyingine 14 zinawania kucheza fainali hizo. Timu nyingine zinazowania ni
Cape Verde v Senegal
Uganda v Misri
Liberia v Morocco
Kenya v Ghana
Msumbiji v Madagascar
Sudan v Libya
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni