Nchi ya Ufaransa imeichakaza bila ya
huruma Iceland na kumaliza ndoto za taifa hilo kufanya miujiza katika
michuano ya Euro 2016 kwa kuifunga magoli 5-2 huko Marseille na sasa
watavaana na Ujerumani Alhamisi.
Ushindi huo ulikuwa wa kushtua na
uliwafanya mashabiki wa wenyeji Ufaransa wakiwa hawaamini macho yao
katika dimba la Stade de France pale walipokuwa kuwa wakiongoza kwa
magoli 4-0 hadi mapumziko.
Shuti la chini la Olivier Giroud na
kichwa cha nguvu cha Paul Pogba akiunganisha mpira wa kona vilitosha
kuwafanya Ufaransa waongoze kwa magoli mawili, kisha Dimitri Payet
alifunga goli la tatu na Antoine Griezmann akafunga la nne.
Iceland ilizinduka katika kipindi
cha pili pale Kolbeinn Sigthorsson alipounganisha kona ya Gylfi
Sigurdsson na kuandika goli la kwanza, kabla ya Oliver Giroud kufunga
goli la tano kwa Ufaransa, huku Birkir Bjarnason akifunga goli la
pili la Iceland.
Paul Pogba akiwa juu baada ya kupiga kichwa cha nguvu kilichojaa wavuni
Dimitri Payet akiangalia shuti lake aliloachia na kujaa wavuni
Mashabiki wa Ufaransa wakishangilia kwa nguvu ushindi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni