Timu
ya taifa ya Ujerumani imetinga nusu fainali za michuano ya Euro 2016,
baada ya kushinda kwa mikwaju ya penati 6-5 dhidi ya Italia katika
mchezo uliojezwa jana usiku mjini Bordeaux, Ufaransa.
Kikosi
hicho cha Joachim Low, mabingwa wa kombe la dunia kilionesha nia ya
kushinda mchezo huo pale Mesuit Ozil alipopachika goli la kwanza
katika dakika ya 65.
Hata
hivyo Italia hawakukata tamaa na uzembe uliofanywa na beki Jerome
Boateg wa kushika mpira pasipo kuwa na sababu, uliwafanya wasawazishe
kwa penati Leonardo Bonucci na kufanya matokeo kuwa 1-1.
Leonardo Bonucci licha ya kupata penati ndani ya dakika 90, alikosa penati katika hatua ya mikwaju ya penati
Wachezaji wa Italia wakiwa wameduwaa baada ya kutolewa kwa mikwaju ya penati na Ujerumani
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni